Saturday, September 12, 2015

Anonymous

Hatima ya YANGA SC na Mastaa Toka Nje Iliyowasajili!

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF lilianzisha sheria ya kuvitaka vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara, kulipa dola 2000 kwa kila mchezaji wa kigeni ili apate leseni. Sheria hii ilikuwa ngumu kidogo kwa vilabu kuiunga mkono, kwani dola 2000 kwa kila mchezaji ni kiasi kikubwa ukizingatia kuna baadhi ya vilabu vina miliki mchezaji wa kigeni zaidi ya mmoja. 

September 11 ripota wa millardayo alipata nafasi ya kukutana na kufanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha, ambapo klabu yao ina wachezaji wengi wa kigeni vipi kwa upande wao wamefanya maamuzi gani kuwalipia au? 

“Kwa hali ya kawaida ilikuwa suala gumu kwa vilabu kukubali kulipa dola 2000, ila tumeona hata kama tukisema tunapinga, tutakosa point sasa hivi mfumo wa vilabu kwa Tanzania ni lazima ipate leseni, ili uweze kupata leseni ya klabu kuna kitu kinaitwa kiapo kutoka CAF, ambacho unapaswa kuheshimu maamuzi ya shirikisho, hivyo tumekubali kulipa licha ya kuwa hatukushirikishwa wakati sheria ikitungwa”>>> Tiboroha

Barua ambayo kipengele (a) inaeleza kuheshimu maamuzi ya Shirikisho la nchi husika. Ndio kilichowafanya Yanga wakubali kulipa dola 2000 kwa kila mchezaji wa kigeni.
Hii hapa chini ni ni sauti ya Tiboroha, waweza bonyeza play kusikiliza au download kuipakua!
-via milardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.