Peter Okoye akiwa na mkewe.
KILA mwanaume anatamani kuwa na mpenzi mzuri, lakini linapokuja suala
la mapenzi kigezo cha uzuri wa mtu huweza kuwa na tafsiri pana kiasi
kwamba wahenga hawakukosea waliposema kipendacho roho hula nyama mbichi
huku Wazungu wakiwa na usemi wa: ‘Beauty is in the eyes of the beholder’
wakiwa na maana kwamba uzuri upo ndani ya macho ya mtu atazamaye.
Lakini misemo yote hiyo bado haiwezi kutengua ukweli kwamba kuna
baadhi ya watu huwa wazuri kiasi kwamba uzuri wao unajidhihirisha wazi
kwa idadi kubwa ya watu wanaowatazama, vivyo hivyo wapenzi wa mastaa wa
baadhi ya mastaa wa kiume barani Afrika, wamekuwa wakitajwa kuwa ni
wazuri zaidi Afrika, baadhi yao ni:
PAUL OKOYE Ni pacha wa Peter
Okoye,pamoja wanaunda kundi la muziki la P.Square nchini Nigeria.
Paul Okoye akiwa na mkewe.
Mwanamuziki huyu ametajwa kuwa na mke mzuri aitwaye Anita Isama
ambapo safari yao ya mapenzi ilianzia tangu wakiwa chuo kikuu na kufikia
kuoana 2014. Ukimuacha Paul, ukoo huo wa Okoye unatajwa kuwa mvuto wa
wanawake wazuri ambapo Peter na kaka yao Jude wote wanatajwa kuwa na wake
wazuri lakini hawamshindi mke wa Paul.
Jose Chameleon akiwea na mkewe.
CHAMELEONE Mkali wa miondoko ya Afro Beat kutoka Uganda,Chameleone
ameingia katika listi ya mastaa wenye wapenzi wazuri kupitia mke wake
ambaye anafahamika kwa jina la Daniella aliyemuoa mwaka 2008, japokuwa
ndoa yao inasuasua kutokana na kile kinachotajwa kama usaliti wa mapenzi
unaofanywa na Chameleone lakini wawili hao bado wapo pamoja hadi hivi
sasa huku wakiunganishwa na mtoto wao anayechipukia kwenye muziki kwa
jina la T-Rex.
BEBE COOL Watu wengi huenda wasifahamu kuwa mkali wa Reggae kutoka
Uganda, Bebe Cool ana mke mzuri aitwaye Zuena aliyezaa naye watoto
wanne. Wawili hawa walioana mwaka 2014 baada ya kuishi bila kufunga ndoa
kwa miaka 12, pamoja wamepitia mengi lakini kuwa kwao pamoja hadi hivi
leo kunaonesha jinsi gani wanapendana.
DIAMOND
Staa huyu kutoka TZ,ambaye ana ‘CV’ ya kutoka na ‘watoto’wazuri,
alianza kama utani baada ya kutoka na mwanamama mrembo kutoka Uganda,
Zari ambaye wakati huo uhusiano wao waliuficha kwenye kile walichokiita
‘Project’.
Baadaye project hiyo ikahamia chumbani zaidi na hatimaye wakapata
mtoto (Tiffah) na kuishi pamoja.ICE PRINCE Rapa huyu kutoka Nigeria
alitambulishwa Tanzania kupitia ngoma aliyoshirikishwa na mwanadada
mrembo Bongo, Jokate Mwegelo inayoitwa Leo Leo,anatajwa kuwa na demu
mkali anayejulikana kwa jina la Maima ambaye ni raia wa Ghana.
motomoto.
WIZKID Mkali huyu wa kibao cha Ojuelegba naye anaingia kwenye
listi ya mastaa wenye wapenzi wazuri kupitia demu wake chotara ambaye ni
muigizaji anayefahamika kwa jina la Tania.
Note: Only a member of this blog may post a comment.