Mwanafamilia wa Hadeel al-Hashlamon akilia kwa uchungu mara baada kumpoteza nduguye.
Picha inaonyesha wakati ambapo askari wa
Israel mwenye silaha akijitayarisha kumpiga risasi msichana wa
Kipalestina (aliyevaa nikabu) sekunde chache baada ya msichana huyo
kujaribu kumchoma kisu mlinzi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi
Magharibi.
Hadeel al-Hashlamon, mwenye umri wa
miaka 18, alipigwa risasi jana katika Ukingo wa Magharibi baada ya
kudorora kwa usalama katika eneo hilo kabla ya kuadhimishwa kwa sikukuu
za Wayahudi na Waislam wiki hii.
Picha zilizochukuliwa muda mfupi kabla
ya msichana huyo kuuawa zinaonyesha jinsi askari wasiopungua wawili wa
Israel walivyokuwa wamemlenga na bunduki zao kabla ya kuuawa kwake.
Jeshi la Israel lilithibitisha mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Hebron ulio katika Ukingo wa Magharibi.
Msichana huyo aliyekuwa anasoma chuo
kikuu, alikimbizwa katika hospitali moja nchini Israel akiwa mahututi
ambapo baba yake, Salah al-Hashlamon, alisema baadaye kwamba alifariki
kwa majeraha. Askari aliyemuua hakupata madhara yoyote.
NA DAILYMAILY
Note: Only a member of this blog may post a comment.