Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

LOWASSA Tunakutaka Wewe, Lakini Mbona Uko Kimya? Wanakusema Sana Lakini Wewe Hujibu Kunani?

Amekutaja na kukusema kimafumbo, Prof. Lipumba wa CUF, umekaa kimya. Hukutoka kujibu. Akakusema kimafumbo rafikiyo Rais Kikwete pale Viwanja vya Jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni zetu, ukanyamaza. Alikuita kuwa una makandokando.Amekutaja Dr. Slaa aliyekuwa CHADEMA na kukutupia makombora ya hasara lakini umekaa kimya.

Wanakusema na kukutajataja wanatimu wa kampeni za CCM kila uchao na kila wapitapo,uko kimya. Husemi kitu. Amekutuhumu na kukuripua Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ukakaa kimya.Badala yake wanajibu akina Lissu, Mbowe, Askofu Gwajima na kadhalika. Madongo yote unalengwa wewe Edward Ngoyai Lowassa.

Yapo yanayokupata na yanayokukosa. Lengo letu watoa madongo na washabikia madongo hayo ni wewe. Tunakutaka wewe ujibu hadharani ili tujibizane nawe na uache kampeni zako kwa muda. Mbona uko kimya? Unatupuuza,unatudharau au unatuvutia mafuta? Sema!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.