Tumezoea kusikia mishahara ya wachezaji soka barani Ulaya kuwa mikubwa ila wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini mastaa kadhaa kutoka Ulaya wamekuwa wakikimbilia Ligi Kuu Marekani (MLS)? wengine usema wanafuata mishahara wengine usema Ligi Kuu Marekani (MLS) ni Ligi ya wastaafu.
September 23 nakuletea list ya mishahara ya mastaa wa soka waliowahi kucheza soka katika Ligi mbalimbali pendwa barani Ulaya, huenda ulitamani kujua mshahara wa mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or wa mwaka 2007 Ricardo Kaka ambaye amewahi kutamba katika vilabu vya AC Milan na Real Madrid.
Nakusogezea list ambayo imeandikwa na mtandao wa metro.co.uk ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika Ligi Kuu Marekani.
1- Ricardo Kaka
Ricardo Kaka analipwa mshahara wa dola milioni 6.6 na klabu yake ya Orlando City kwa mwaka.
2- Steven Gerrard
Steven Gerrard anayeitumikia klabu ya LA Galaxy analipwa mshahara wa dola milioni 6.2 kwa mwaka.
3- Frank Lampard
Kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya New York City FC Frank Lampard analipwa dola milioni 6 kwa mwaka.
4- Michael Bradley
Michael Bradley anayecheza klabu ya Toronto FC analipwa sawa na Lampard dola milioni 6 kwa mwaka.
5- David Villa
David Villa wa klabu ya New York City analipwa dola milioni 5.61
6- Sebastian Giovinco
Sebastian Giovinco analipwa na klabu yake ya Toronto dola milioni 5.6.
7- Jozy Altidore,
Jozy Altidore analipwa dola milioni 4.75 kwa mwaka katika klabu ya Toronto FC .
8- Robbie Keane
Robbie Keane wa LA Galaxy analipwa dola milioni 4.5 kwa mwaka.
9- Giovani Dos Santos
Giovani Dos Santos wa LA Galaxy analipwa dola milioni 4 kwa mwaka
10- Clint Dempsey
Clint Dempsey kutokea klabu ya Seattle Sounders analipwa dola milioni 3.9.
Hii ni list ya wachezaji wote 18 wanaolipwa fedha nyingi na vilabu vyao katika Ligi Kuu Marekani (MLS)
Note: Only a member of this blog may post a comment.