Sunday, September 20, 2015

Anonymous

KAULI TATA za Viongozi Wa CCM, Kukimbia Kampeni, Kujilimbikizia Majimbo: Freeman MBOWE wa CHADEMA Afunguka!



Umoja wa katiba ya wananchi ukawa umeitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha inakichukulia hatua kazi za kisheria chama cha mapinduzi CCM kwa kutumia kauli zinazoweza kuhatarisha hali ya amani hasa wakati huu wa kampeni za uchgauzi mkuu wakati watanzania wakisubiri kufanya maamuzi ya nani atayerithi kiti cha rais Kikwete kwa misingi ya kikatiba.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema ameelezea kusikitishwa na kauli tata iliyotolewa na moja ya kiongozi wa juu wa CCM katika mkutano wa hadhara mkoani Kigoma ambapo amesema kauli hiyo ya kibabe inatokana na sheria kandamizi za Uchaguzi.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, amaeelezea baadhi ya tuhuma kadhaa ambazo zilielekezwa na baadhi ya viongozi wa NCCR mageuzi juu ya Chadema kujilimbikizia majimbo mengi ya uchaguzi, jambo ambalo amesema kanuni na taratibu za ugawanaji majimbo zilifuatwa.

Kwa siku kadhaa kumekuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii zikionyesha mazungumzo ya Email kati ya mwenyekiti huyo na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, huku taarifa nyingine zikisambazwa kuwa mwenyekiti huyo amekimbia kampeni taarifa ambazo pia amezikanusha.

Hayo yanajiri siku moja kabla ya mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema ambaye anatarajiwa kuanza kunguruma jijini Dar es Salaam mapema Sep 20 kabla ya kuongoza harambee ya uchangaiji wa fedha za kampeni zinazofanywa na Chadema huku zikiungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.