Kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal, meneja Jose Mourinho ametamba kumaliza uteja wa kushindwa kupata point nyumbani tangu mwanzoni mwa msimu huua ambapo mashabiki wameshuhudia wakiambulia alama moja wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea City kufuatia sare ya mabao mawili kwa mawili.
Amesema anaamini Arsenal watakwenda kwa lengo la kutaka kuendeleza matokeo mabaya kwa Chelsea lakini amesisitiza haoni sababu ya jambo hilo kutokea tena kutokana na kikosi chake kuwa vizuri kwa sasa.
Meneja huyo kutoka nchini Ureno, amesema mchezo huo utakua na upinzani mkubwa kutokanana kumbukumbu ya mpambano wa kuwania ngao ya jamii ambapo The Blues walikubali kupoteza kwa bao moja bila majibu dhidi ya Arsenal mwanzoni wma mwezi uliopita, hali ambayo anaamini inapaswa kulipiziwa kisasi.
Hata hivyo hakuona uchungu kukumbushia matokeo mabovu yaliyomkumba, kwa kusema ni vigumu kuamini mpaka sasa kama amepoteza michezo mitatu dhidi ya Crystal Palace, Everton pamoja na Man City hivyo itamlazimu kila mmoja wao kuchukulia hali hiyo kama sehemu ya kuhakikisha wanamaliza dakika 90 za mpambano wa kesho kwa furaha.
Chelsea watakua nyumbani hiyo kesho huku wakiwa katika hali mbaya ya kujiuliza kwa nini mpaka hivi sasa wanakamata nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England huku wakimili point 4 baada ya kucheza michezo mitano ambayo ilishuhudia wakipoteza mitatu, wakishinda mmoja na kupata sare mara moja. Wapinzani wao Arsenal wapo katika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia point kumi baada ya kucheza michezo mitan

Note: Only a member of this blog may post a comment.