Saturday, September 26, 2015

Anonymous

Je, Umeshawahi Kujiuliza Kama Kuna Ugomvi Wowote Kati ya LULU na WEMA? Lulu Afunguka Haya...


KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepetu, utakuwa umekosea, kwani hakuna ugomvi kati yao.
Lulu alieleza kwamba wamekuwa wakishirikiana na Wema Sepetu katika mambo mbalimbali, ikiwemo sherehe, misiba na mijumuiko mbalimbali
“Nampenda Wema kama dada yangu na yeye ananipenda vile vile, nimekuwa nikihudhuria kwenye shughuli mbali mbali ambazo zinamhusu, nilishiriki vema katika msiba wa baba yake na sherehe zake mbalimbali,” alisema.
Lulu na Wema ni wasanii waliokumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya sanaa, lakini wameweza kuendeleza umaarufu wao hadi sasa na wamejizolea idadi kubwa ya mashabiki.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.