Ameahidi kuboresha hali za wanajeshi, walimu na wafanyakazi nchini.
Mgombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli
akijinadi kwa wananchi katika Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga jana
wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.
Sehemu ya umati wa wananchi ulifurika kwenye mkutano huo wa kampeni katika Jimbo la Bumbuli
Mtoto
akiimba kwa ufasaha wimbo wa kuhimiza watu kwenda kupiga kura Oktoba
25, mwaka huu na kumpigia kura Dk Magufuli ili ashinde urais.
Dk
Magufuli akiwa amembeba mtoto huyo baada ya kufurahishwa na uimbaji
wake katika mkutano wa kampeni Kata ya Malamba, Wilaya ya Nkinga.
Mmoja wa wazee wa Kata ya Malamba akiwa na furaha baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli.
Msanii Joti wa kikundi cha uchekeshaji cha The The Orijino Komedi akimchukua Dk Magufuli ili ajumuike nao kucheza muziki wakati wa kampeni hizo.
Dk Magufuli akijumika kucheza muziki na wasanii wa kikundi cha The Orijino Komedi
Baadhi ya wazee wa Kata ya Malamba, mkoani Tanga, wakiwa na picha za Dk Magufuli
Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Nkinga
Baadhi
ya vijana wakishangilia baada Dk, Magufuli kutoa ahadi kuwa akishinda
Serikali yake itakuwa inatoa kwa kila kijiji sh. mil 50 kwa wazee na
vijana kwa ajili ya mikopo ya kuanzishia miradi ili wajikimu kimaisha.
Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika Kijiji cha Mashewa
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ‘Prof Maji Marefu”
Akimpunia mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli.
Mfuasi
wa CCM akishangilia kwa furaha baada Mgombea urais, Dk Magufuli kuahidi
kwamba akishinda wataanzisha utaratibu wa kuwakopesha wanawake na
Vijana kwa kila kijiji kupatiwa shmil 50. Mkutano huo wa kampeni
umefanyika katiuka Kata ya Matalawanda.
Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi, mgombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani
Wafuasi wa CCM wakiwa wameshikilia bango hilo katika mkutano wa kampeni mjini Korogwe
Katibu
Mkuu msitaafu, Yusufu Makamba akielezea sifa lukuki alizonazo Dk
Magufuli tofauti na mgombea kupitia Umoja wa Katiba ya wananchi
Dk Magufuli akiteta jambo na January Makamba
Wasani wa The Orijino Komedi wakilishambulia jukwa wakati wa mkutano huo
Mwakilishi
wa watu wenye ulemavu Amon Mpanju akielezea jinsi CCM inavyo wajali
watu wa namba hiyo wakati wa mkutano mjini Lushoto jana
Dk Magufuli akimtambulisha kwa wananchi Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba
Wagombea udiwani Jimbo la Bumbuli wakitambuliwa kwa wananchi katika kkiutano huo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu akimnanga Frederick Sumaye kwa ni fisadi zaidi ya Lowassa.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mlalo, Hassan Ngwilizi akimpigia chapuo Dk Magufuli katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya kaampeni ya CCM, Ummy Mwalimu akimpigia debe Dk Magufuli wakati wa mkutano huo
Dk Magufuli akijinadi mjini Lushoto.
Akishinda urais Dk Magufuli
amehidi kujenga barabara ya lami kutoka Soni hadi Bumbuli yenye umbali
kwa Km 22. Pia ameahidhi kuharakisha mchakato wa kukikabidhi kiwanda cha
chai cha Mponde kwa wananchi na kuanza kuzalisha.
Pia ameahidi kuboresha hali za wanajeshi, walimu na wafanyakazi nchini.
Dk Magufuli ambaye kampeni zake huzifanya kwa magar, tayari hadi sasa kafanya katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Morogoro na Tanga na leo anaanza kampeni katika Mkoa wa Mara.
Dk Magufuli ambaye kampeni zake huzifanya kwa magar, tayari hadi sasa kafanya katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Morogoro na Tanga na leo anaanza kampeni katika Mkoa wa Mara.
NA RICHARD MWAIKENDA WA MATUKIO BLOG

Note: Only a member of this blog may post a comment.