Ronke na Lawson wamependana?
Love yao hawakutaka masuala ya kusumbuana na ndugu masuala ya michango,
vikao vya Harusi, kujaza watu Ukumbini.. wao kila kitu kimefanywa
simple tu yani.
Jumapili ya September 13 2015 mambo yalikuwa motomoto kwenye Beach moja Lagos Nigeria, Ronke na Lawson walifunga Ndoa yao kwa mtindo wa aina yao kabisa yani !!
Ndoa ilifungwa kwa wapenzi hao kula
viapo walivyobuni hapohapo tena wao wenyewe, hakuna pete wala Mchungaji
wa kufungisha Ndoa… Badala ya pete, Bibi Harusi alivalishwa cheni ya
dhahabu na mumewe, bwana harusi nae akavalishwa soksi na mkewe, mambo
yakaendelea !!
Wageni waalikwa list hata haikuwa ya
kuumiza vichwa, walialikwa ni watu nane tu… unaambiwa kwenye hao nane na
mpiga picha nae kahesabiwa humohumo.
Mambo ya After Party je
??? Iliishia hivi, bibi harusi na bwana harusi walijiachia kwenye maji
wakaogelea alafu mambo ndio yameisha hivyo, Bibi na Bwana wanaendelea na
maisha mdogomdogo !!
Dunia ina mambo yake mdau, unatamani na wewe ungeishuhudia hii mdau wangu??

Note: Only a member of this blog may post a comment.