Chama cha soka nchini England FA, kimemfungulia mashataka ya kinidhamu meneja wa klabu bingwa nchini humo Chelsea, Jose Mourinho baada ya kubaini alimnyanyasa kijinsia daktari wa kikosi cha The Blues, Eva Carneiro wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi mwezi uliopita.
Gazeti la The Independent, liliandika taarifa za tukio hilo na kuanika wazi maneno yaliyotamkwa na meneja huyo dhidi ya daktari Eva, na yalionyesha dhahir yalikua yakimnyanyasa kijinsia.
Mundiashi wa taarifa hizo, Sam Wallace alikwenda mbali zaidi na kukitaka chama cha soka nchini England FA, kuchunguza kwa kina tukio hilo na ikibidi kumuadhibu Mourinho kwa tamko alilomtolea daktari huyo wa kile.
Kutokana na hali hiyo inahisiwa FA wamepata msukumo wa kuingilia kati na kufanya uchunguzi wao ambao umebaini jambo, lililopelekea kumfungulia mashataka Jose Mourinho.

Note: Only a member of this blog may post a comment.