Stori: Na Richard Bukos, Kagera
NIKO fiti!
Ndivyo alivyosema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John
Pombe Magufuli kuudhihirishia umma kwamba yupo fiti kimazoezi.
Tukio hilo lililoibua shangwe ya aina
yake lilijiri juzi, Jumanne katika Viwanja vya Kayanga, Wilaya ya
Karagwe, mkoani Kagera wakati Magufuli alipokuwa akiendelea na ziara
zake za kampeni.
Mara baada ya kuwahutubia maelfu ya
wakazi wa mkoa huo kwa kuwaeleza sera na ilani za chama chake, mgombea
huyo ambaye amejijengea sifa ya ukakamavu kwa kupanda jukwaani kwa
staili ya kukimbia mithili ya mwanariadha, aliwaambia wananchi wamchague
yeye kwani yuko fiti.
“Msije mkachagua watu wenye afya
mgogoro, wanaoshindwa kupanda jukwaani, wasiojua kuongea mpaka watembee
na washenga wa kuwazungumzia…mgombea unatakiwa uwe fiti kama mimi.
Wakati akipiga push up, umati wa watu
ambao ulifurika katika viwanjani hivyo ulisikika ukihesabu,
moja…mbili..tatu na kuendelea huku wengine wakisema:
“rais…rais…rais…rais..rais…”
Katika hotuba yake, Magufuli aliyekuwa
akijinadi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa
alisema wakulima wa kahawa waliopo eneo hilo atawafutia kodi mbalimbali
ambazo zinamfanya mkulima asiambulie kitu baada ya kuuza.
Alisema katika kila kijiji cha wilaya
hiyo ataanzisha mifuko ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukopesha
wakazi wa eneo hilo huku akiahidi kutengeneza barabara ili kurahisisha
usafiri katika mitaa yao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.