Kuna wakati ambao ikitokea mambo
yameharibika angani, Rubani wa ndege anaamua kufanya maamuzi magumu ili
kuokoa abiria wake na kuhakikisha hakiharibiki kitu.
Nimekipata kipande cha video ya kama
sekunde 72 hivi, jamaa walikuwa wanaendesha zao magari kwenye barabara
Mitaa ya California, Marekani… wakati wamefika kwenye mataa wakasimama
kusubiri kuruhusiwa kuvuka, ghafla ikakatisha ndege ndogo speed kabisa,
ikaenda mbele ikasimama !!
Ripoti ya Polisi haijasema sababu ya
ndege hiyo kutua kwenye barabara ya magari, ila ndani ya ndege kulikuwa
na Mwalimu pamoja na Wanafunzi wanaojifunza Urubani.. wote walitoka
salama na ndege ilitua salama kabisa, hakukuwa na athari yoyote
iliyojitokeza japo ni mara chache sana ndege kutua mazingira kama hayo
alafu isitokee tatizo.
Unaweza kuplay hizi video kuona hali ilivyokuwa mpaka ndege ikatua barabarani.
Hiki hapa kipande kingine cha video chenye mwendelezo wa tukio hilohilo
Hiki hapa kipande kingine cha video chenye mwendelezo wa tukio hilohilo

Note: Only a member of this blog may post a comment.