Saturday, August 1, 2015

Anonymous

VIOJA VYA BVR DAR: MKE AVULIWA NGUO ZOTE HADHARANI NA MUMEWE, ALA KICHAPO NA KUTIMULIWA USIKU NA KICHANGA!

13.BVRMwandikishajiakichukuataarifakamilizammojawawananchiwalioendakujiandikisha..JPGUandikishaji BVR
Hamida Hassan
VIOJA! Zoezi la uandikishaji wa wapigakura katika daftari la kudumu unaoendelea jijini Dar es Salaam juzi kati ulimponza mwanamke mmoja, Mama Khadija baada ya kupigwa vibaya na mumewe kisha kufukuzwa, baada ya kuchelewa kurudi nyumbani akitokea kituoni kujiandikisha.

Akizungumza na gazeti hili kwa taabu, mwanamke huyo alisema mumewe aliyemtaja kwa jina la Baba Khadija, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam, alimuumiza taya na shingo, huku akimvua nguo zake zote alizovaa na hivyo kumuacha utupu mbele ya umati wa watu.

“Nakumbuka siku ya kwanza nilimwambia mume wangu nimekwenda kule kuandikisha, nimekuta watu wengi nimepewa namba 15 na nimeambiwa nirudi kesho yake, akanijibu sawa, akaniambia na yeye atakuwepo nyumbani siku hiyo haendi kazini,” alisema mama huyo.

Lakini kesho yake alipofika katika kituo cha uandikishaji, zoezi hilo lilichelewa kuanza, lakini hata hivyo, kwa muda wote alikuwa akiwasiliana na mumewe hadi alipomaliza na kupata kitambulisho chake kisha kurejea nyumbani.

BVR 
Mama Khadija anayedaiwa kupigwa na mumewe. 
“Nilishangaa alipokuja usiku wa saa tatu na nusu mume wangu alianza kunipiga, nilikuwa nimevaa kanga mbili akanivua watu wakajaa ikiwa ni pamoja na watoto, kisha akanifukuza nyumbani kwake na mtoto wangu wa miaka miwili na miezi saba, aliniuliza kama na mimi siku hizi nimekuwa mwanasiasa,” alisema.

Baada ya kupigwa, alikimbilia serikali ya mtaa na baadaye kwa mwanaharakati Janet Mbeo ambaye alimpa hifadhi kwa usiku huo akiwa na mwanaye kisha akalifikisha suala hilo Polisi Oysterbay kwa mkuu wa dawati la Jinsia, Afande Prisca kwa ajili ya kulishughulikia kisheria.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.