Saturday, August 1, 2015

Anonymous

Hatimaye LOWASSA Afungukia Tuhuma za Uchu wa Madaraka! Awajibu Wanaomtukana Kwa Kuhama CCM!

lowassa2.jpg 
WAZIRI mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Brighton Masalu
WAZIRI mkuu wa zamani, Edward Lowassa amefungukia kile kinachoitwa “uchu wa madaraka” kwa kusema wanaomchafua kwa kumtangaza kuhama chama kwa kigezo hicho, wanajidanganya kwani amedhamiria kutafuta mabadiliko ya kweli nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza mbele ya wanachama wa chama chake kipya (Chadema) na waandishi wa habari Alhamisi ya wiki hii wakati wa kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chama hicho ndani ya umoja wa vyama vya upinzani (Ukawa), Lowassa alisema kuna minong’ono na maneno ya uongo yanayoenezwa mitaani kuwa, chanzo kikubwa cha kuchukua uamuzi wa kuhama CCM ni uroho na uchu wa madaraka.

Alisema, kilichomsukuma kuhama chama, ni kuona haki haitendeki ndani ya CCM, pia alifuata msemo wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
“Wanaonitukana kuwa nimehama chama kwa sababu ya uchu wa madaraka, wakidhani kuwa nitayumba, wanajidanganya, kamwe siyumbi wala sitetereki kwa kuwa nafuata kauli ya mwenyekiti wa taifa hili Mwalimu Nyerere ya kuyatafuta mabadiliko nje ya CCM,” alisema Lowassa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.