Na Omary Mdose
COASTAL Union imetangaza kumsajili
kiungo wa zamani wa Simba, Ibrahim Twaha ‘Messi’ kwa mkataba wa miaka
miwili, utata umeibuka juu ya usajili huo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa Messi aliliambia gazeti hili kwamba, kiungo huyo amesaini mkataba wa miezi minane tu kisha aende Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa.
“Viongozi wanatangaza Messi kasajiliwa na Coastal miaka miwili, siyo kweli kwani ukweli ni miezi minane tu kwani anataka kwenda kujiunga na klabu moja huko Afrika Kusini,” alisema rafiki huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.