Hans Mloli,Dar es Salaam
PALE Simba SC kwenye safu ya kiungo kwa sasa hakukaliki na kama ukicheza unaweza kuozea benchi kulingana na mafundi waliojazana kwenye safu hiyo, kwa kuligundua hilo, kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Peter Mwalyanzi, ameamua kuongeza muda wa ziada wa kufanya mazoezi ili awe bora zaidi ya wenzake.
Mwalyanzi aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Mbeya City, kulingana na nafasi anayocheza amekiri kuwa imemlazimu aandae ratiba mpya ya kufanya mazoezi ya peke yake ili akae sawa na aweze kwenda sawa na viungo wengine klabuni hapo.
Ukitoa Mwalyanzi, Simba inaundwa na viungo wengine ambao wote wana uwezo wa kukaba na kuchezesha timu, wakiongozwa na Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Awadh Juma, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla na Mzimbabwe, Justice Majabvi aliye kwenye mazungumzo na Simba kabla ya kuingia kandarasi.
“Kwa kweli kuna kazi kubwa, katika kiungo hapa ndiyo naona kuna ushindani mkubwa sana halafu mifumo mingi hutumia viungo wawili au watatu, kwa hiyo ni lazima nipambane kupata nafasi hapo, nimeamua kujiongezea muda wa mazoezi ili niwe sawa zaidi.
“Yaani nikitoka kwenye mazoezi ya timu ambayo nitayazingatia sana maana ndiyo msingi wenyewe, baada ya hapo nitaingia kwenye programu zangu binafsi,” alisema Mwalyanzi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.