Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa
mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City
katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa
ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia
madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama
cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo
mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na
Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha
mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa
nchini.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka
na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha ndani ya ukumbi wa Mlimani
City katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii
kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia
madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama
cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini
Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea
Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape
Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na
wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City
kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa
ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia
madarakani kwa miaka 10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama
cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul
Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya
kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru
kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete
akifurahia jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr
John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini
Dar.
Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom, Kelvin Twisa.
Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa Bongo fleva.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city.
Wanauziki wakongwe pia walikuwepo
kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake
wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki.
Mmoja wa wasanii akiimba jukwaani kwa hisia.
Baadhi ya Wanamuziki wakongwe walihudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Wanamuziki wakongwe pia walikuwepo
kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake
wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki.
Mmoja wa wasanii akitumbuiza jukwaani.


































Note: Only a member of this blog may post a comment.