Monday, August 10, 2015

Anonymous

PICHAZ NYINGINE: Shuhudia Barabara zilivyofungwa Dar baada ya Lowassa kuchukua Fomu ya Urais NEC leo....



Headlines za Siasa zinaendelea kubeba uzito wa juu Tanzania, August 10 2015 Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa amefika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kuchukua Fomu yake.

Pichaz za kwanza nilikusogezea msafara uliotoka Makao Makuu wa CUF Buguruni Dar es Salaam, wengine kwenye magari, wengine bodaboda.. wengine walifunga safari kwa miguu kumsindikiza Mgombea huyo kutoka Buguruni mpaka Ofisi za NEC Posta alafu safari ikaendelea tena mpaka Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni Dar.

Ilionekana watu ni wengi sana, nafasi ya eneo hilo haikutosha… ikabidi umati wote usogee Viwanja vya BIAFRA ambapo Viongozi wa UKAWA walipata nafasi kuongea na Wanachama wao walioshiriki mwanzo mpaka mwisho kwenye safari hiyo.








Hapo yuko Freeman Mbowe, Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa, na James Mbatia.

Mwimbaji Frola Mbasha.

Maalim Seif Shariff Hamad.






Hii ni barabara ya Uhuru, msafara umetokea Buguruni kuitafuta Ilala, Kariakoo mpaka Posta.

Watu wa Usalama nao wako hatua kwa hatua kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.





Hapa ni Ilala Boma, Dar es Salaam.. Msafara unaendelea.






Hapa ni mitaa ya Ilala, wengine kwenye Bodaboda wengine wako kwa miguu.


Wabunge Godbless Lema na Mchungaji Peter Msigwa.


Hawa nao hawakutaka kupitwa, wakakaa juu juu waone kinachoendelea mtaani.

Camera zote zikageuziwa kwenye mlango wa Tume ya Uchaguzi NEC.

Wabunge wanne walisafiri hivi wenyewe, aliyekaa mbele ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wa juu ni Godbless Lema, Peter Msigwa na Joshua Nassari.

Gari imejaa ndani, wengine wamekaa juu na wengine wananing’inia.

Tundu Lissu na Freeman Mbowe wao walikaa juu ya gari na safari inaendelea kuelekea Kinondoni.




Mapokezi yalikuwa hivi kwenye Viwanja vya BIAFRA, K’ndoni Dar.


Huu ni muonekano wa juu kwenye msafara huo, hii picha nimeitoa kwenye ukurasa wa Instagram wa Jackline Wolper

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.