Monday, August 10, 2015

Anonymous

NICKI Minaj Atangaza ni Mjamzito! Baba wa Mtoto Huyu Hapa....

Rapa wa kike aliyejizolea umaarufu kutoka lebo ya Cash Money, Nicki Minaj.
Burgettstown, Pennsylvania
RAPA wa kike aliyejizolea umaarufu kutoka lebo ya Cash Money, Nicki Minaj hivi karibuni ametangaza kuwa ni mjamzito.
Nicki (32) aliweka wazi alipokuwa jukwaani katika tamasha kubwa lililojumuisha ziara yake ijulikanayo kama Pinkprint huko Pennsylvania ambapo alipanda na mchumba wake, Meek Mill na kusema;
“Piga kelele kwa baba wa mtoto wangu!”
Baada ya shoo hiyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nicki aliweka kipande cha video hiyo akizungumza maneno hayohayo sambamba na kuambatanisha kikatuni (emoji) ya kulia. 

Kwa kipindi kirefu Nicki amekuwa na uhusiano na Meek Mill ambapo hivi karibuni uhusiano wao ulidaiwa kuteterereka kwa kile kilichoelezwa ni kutupiana matusi kwa Meek na Drake kwenye nyimbo zao na mitandao ya kijamii.
Hongera Nicki kwa ujauzito ulionao!
(Imeandaliwa na Andrew Carlos kwa msaada wa mtandao)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.