Monday, August 10, 2015

Anonymous

MSIBA MZITO UKAWA! Mbunge Huyu Afariki Kwa Ajali Mbaya ya Gari

Clara Mwatuka enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Clara Mwatuka, amefariki dunia leo Jumapili jioni baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuelekea Ndanda, Masasi mkoani Mtwara.
mwatuka gari
Gari alilopata nalo ajali marehemu Mwatuka.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake, ambaye inasemekana ni mwanaye. Maiti ya marehemu Mwatuka imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda.
Viongozi waandamizi wa CUF wamethibitisha kutokea msiba huo.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.