Marufuku ya mitandao ya ngono India yaondolewa!
Serikali ya India imeruhusu mitandao ya filamu za ngono kuwepo baada ya shinikizo kutoka kwa wananchi.
Serikali iliondoa marufuku iliyoweka dhidi ya mitandao 857 ya kupeperusha filamu za ngono.
Idara
ya mawasiliano imewaeleza watoaji wa huduma za intaneti dhidi ya
kufunga kurasa zisizokuwa na video za ngono zinazowadhalilisha watoto.
Waziri Ravi Shankar Prasad alikutana na maafisa wakuu siku ya Jumanne na kutoa uamuzi huo.
Serikali
imepinga kutekeleza hatua za kuweka mpangilio za kimaadili na kueleza
kuwa inawalinda watoto dhidi ya kutazama picha hizo.
Mwezi Julai, mahakama kuu iliishtumu serikali kwa kutofunga mitandao yenye picha za uchi za ngono zinazowahusisha watoto.
Hata hivyo, watoaji wa huduma za intaneti wametofautiana na serikali.
India ilikuwa imeweka amri hiyo kali ilikulinda maswali ya watoto wasidhulumiwe
Msimamizi wa kampuni za kutoa
huduma za mtandao wa intanet amenukuliwa kwenye gazeti la Times of
India akieleza wasiwasi wao kuhusu kuwajibishwa kukagua kurasa zenye
ngono zinazowahusisha watoto.
Taarifa za uondoaji wa marufuku hiyo
zimevutia hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii nchini humo huku
viongozi wa kisiasa wakipinga uamuzi wa serikali kuondoa marufuku.
Aidha Waziri Prasad ameitetea serikali kwa kusema kuwa wanaheshimu uhuru wa vyombo vya mawasiliano.
-BBC


Note: Only a member of this blog may post a comment.