Saturday, August 1, 2015

Anonymous

MONALISA :Wasanii Wa KIKE TZ Wanajiachia Sana!


YVONNE Cherryl ‘Monalisa’ mwigizaji wa kike katika tasnia ya filamu Swahilihood amefunguka kwa kuwaambia baadhi ya wasanii katika fani ya uigizaji kushindwa kulinda miili yao na kujiachia kwa kunenepa na kupoteza muonekano wao jambo ambalo linapoteza nafasi zao katika sinema.
“Sisi wasanii wa filamu kwa Bongo hatuwezi kabisa kulinda muonekano wetu kimaumbo msanii akikubalika tu anajiachia mwili huo, vijana wadogo tu kuna wakati unashindwa umchezeshe kama binti au mama mtu mzima, lakini ukimuona msanii kama Sarafina yupo vile vile,” anasema Monalisa.

Monalisa anasema kuwa moja kati ya vitu muhimu katika tasnia ya filamu ni kuwa na mpangilio wa vyakula kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa katika muonekano mzuri kama vile akina Angelina Jolie walivyodumu na hata badhi ya wasanii wengine Afrika ambao hawajapoteza mvuto kwa kujiachia kunenepa bila mpangilio.
Chanzo: FC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.