Msanii wa filamu za vichekesho, Kingwendu ambaye mwaka huu anawania
ubunge katika jimbo la Kisarawe, amesema akifanikiwa kuingia bungeni
atawatumikia wananchi wa Kisarawe na kwamba atapumzika kufanya filamu
kwa miaka mitano.
Kingwendu amesema anafuata sheria ya kukubali kuwatumikia wananchi na sio kufanya shughuli nyingine tofauti.
“Kazi kubwa nitaifanya kwaajili ya watu wangu walionichagua,” amesema.
“Maji, barabara pamoja na afya ni vipaumbele vyangu. Lakini kwa
upande wa sanaa nitahakikisha msanii anapata haki yake katika kazi
anayoifanya. Tutapambana na wezi wanaotuibia kazi zetu. Ingawa
nitapumzika kufanya kazi za sanaa kwa miaka yote nitakayokuwa bungeni,
lakini nitakuwa pamoja na wasanii katika harakati mbalimbali za
maendeleo.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.