Bondia Floyd Mayweather, 38, ambaye anajiandaa na pambano lake la
mwisho dhidi ya Andre Berto litakalofanyika MGM Granda mjini Las Vegas,
Septemba 12, ameonesha magari yake matano ya kifahari yenye thamani ya
dola milioni 10.6 kwa pamoja katika klabu yake ya masumbwi mjini Las
Vegas, Nevada.
Magari hayo ni pamoja na Ferrari 458 Italia ($300,000), Bugatti
Veyrons mbili (kila moja dola milioni 1.5) na convertible Bugatti (dola
milioni 2.5) na Koenigsegg yenye thamani ya (dola milioni 4.8.)
Floyd alifika kufanya mazoezi akiendesha gari aina ya Koenigsegg
yenye thamani ya dola milioni 4.8. Kuna gari mbili tu za aina hiyo
duniani.
Mayweather akiwasili katika klabu yake ya ngumi mjini Las Vegas, Nevada

Note: Only a member of this blog may post a comment.