Rapper wa Tip Top Connection, Dogo Janja amesema yeye ni miongoni mwa
watu ambao hawawezi kuwaweka wazi wapenzi wao kwenye mitandao.
Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa kitu anachoogopa ni kuanza kutupiana maneno wakati wanapoachana.
“Unajua mapenzi ya kwenye mitandao ukigombana tu na mpenzi wako au
mkikosana, watu wataanza kutupiana maneno ingawa kwa watu wengine
haitokei,” amesema. “Pia unajua kila mtu kalelewa tofauti na mimi sio
kwamba sina girlfriend, mimi naamini katika sanaa yangu watu wamenijua
mimi kama mimi. Ningependa watu waendelee kumjua Dogo Janja. Sometimes
vitu kama hivi vinaweza kukupotezea uaminifu wako, unajua kuna watu
wanatuangalia,” ameongeza rapper huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.