Mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF) amedai kutekwa, kutishwa
na kuporwa fomu za kugombea katika jimbo la Shaurimoyo, Unguja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam.
Mgombea huyo, Abdi Seif Hamad, alidai kuwa tukio
hilo lilitokea Agosti 17, mwaka huu majira ya asubuhi katika maeneo ya
jimbo hilo. Alidai kuwa akiwa maeneo hayo wakati akitafuta wadhamini,
ghafla kikatokea kikundi cha watu wapatao wanane wakiwa wamejifunika
nyuso na kumteka, kumtisha kisha kumnyang’anya fomu ambazo alikuwa
ametoka kuzichukua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
“Namshukuru Mungu hawakunijeruhi wala kunipiga, waliniambia
wanachokihitaji ni fomu ambazo nilizokuwa nimebeba mfukoni,” alidai
Abdi.
Alidai kuwa baada ya kumnyang’anya fomu hizo walimuachia na kwenda
kuripoti kituo cha polisi cha Ng’ambu na kupewa namba RB/6085/2015 kisha
kuripoti Nec na jana alipewa fomu nyingine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema hajapata taarifa za kuripotiwa kwa tukio hilo.
“Watu wangu waliopo katika
doria siku ya mkutano wa Chadema uliongozwa na mgombea wa urais kupitia
chama hicho, Edward Lowassa, ndio walipata taarifa hiyo kutoka kwa
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alitoa taarifa ya
tukio hilo akiwa juu ya jukwaa akiwahutubia wananchi,” Mkadam.
-Nipashe


Note: Only a member of this blog may post a comment.