Tuesday, August 4, 2015

Anonymous

MAGUFULI AITIKISA DAR LEO!

Mhe Magufuli akionesha fomu za kugombea urais mwaka 2015 na Mgombea mwenza, Samiah Suluhu (kulia) wakiwa nje ya Ofisi za NEC mara baada ya kuchukua fomu.
Wagombea hao wakiwa njiani kuelekea Ofisi za CCM zilizopo Barabara ya Lumumba, Dar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa, Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Ofisi za CCM.
Mhe John Pombe Magufuli akizungumza jambo katika mkutano mfupi mara baada ya kutua ofisi za CCM.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe Abdurahman Kinana akizungumza jambo.
Mhe Magufuli na mgombea mwenza, Samiah Suluhu walipowasili katika Ofisi za NEC.
Wagombea hao wakishuka katika gari maalumu la CCM.
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Mhe Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mh Magufuli (katikati).Hali ilivyokuwa katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wakati Mhe John Pombe Magufuli alipowasili katika ofisi hizo kuchukua fomu.Wagombea hao wakipunga mikono kwa wananchi katika barabara walizopita.
Wanahabari wakiwa kazini wakichukua matukio.
Nape Nauye (mwenye kofia) akiwa amejumuika katika gari la wanahabari kuelekea Makao Makuu ya CCM.
Hali ilivyokuwa katika barabara ya Bibi Titi.
JIJI la Dar es Salaam na vitongoji vyake, leo lilisimama kwa muda baada ya mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli na mgombea mwenza, Samiah Suluhu Hassan kwenda katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu kwa ajili ya nafasi hizo.

Wagombea hao ambao wamesababisha mtikisiko mkubwa, walipitia Barabara ya Morogoro, Bibi Titi Mohamed na Ohio kuelekea katika ofisi hizo wakitokea Ofisi za CCM, Lumumba ambapo shughuli kadhaa za watu zilisimama kwa ajili ya tukio hilo huku pia wakionekana kivutio na wananchi kusikika wananchi wakiimba nyimbo mbalimbali.

Mbali na uchukuaji fomu, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk Jakaya Mrisho Kikwete alifika katika ofisi ndogo za chama hicho kwa ajili ya kuwalaki wagombea hao.Rais Kikwete akisema kwamba CCM itarajie ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu.

Wapinzani watarajie anguko na pia ushindi mkubwa kwetu,” alisema Kikwete huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.
 (HABARI/PICHA : DENIS MTIMA NA HARUNI SANCHAWA/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.