Wednesday, August 5, 2015

Anonymous

KWELI TZ TUMEPIGA HATUA! Msanii DIAMOND PLATINUMZ Azua Gumzo Kubwa Katika Mtandao Huu wa Nchini Marekani!



Kiukweli kwasasa huwezi pinga kuwa Diamond Platnumz ni msanii mkubwa na anacoverage kubwa ya mashabiki wa ndani na nje ya Afrika, Kitendo cha kuandikwa na mtandao wa Bossip moja ya mitandao ya gossip inayoongoza nchi marekani sio kitu cha kawaida lakini kitu cha kushangaza zaidi ni jinsi watu walivyouvamia huo mtandao baada ya kumuita Diamond ‘Unknown artist’ 

Mtandao wa Bossip uliandika kuhusiana na tukio lililotokea mwaka jana Club Bilcanas kwenye show ya Queen darling, baada ya shabiki mmoja aliyekua analia baada ya kumwona Diamond, Mbali ya kumwita ‘Unkown artist’ kitendo tu chakuandika habari yake tu ni wazi kuwa Diamond anafatiliwa na watu wengi na wakubwa, unakumbuka Ne-yo alisema alianza kumsikia Diamond kabla hata hajaja kwenye Tuzo za MTV MAMA? unakumbuka Manager wa T.I alivyokuja kwenye Fiesta aliulizwa kama anamjua Diamond na akajibu kuwa amewahi kumsikia, Hii inatosha kuonesha jinsi gani Diamond ni msanii mkubwa kwa sasa.

Mtandao huo wa Bossip uliandika habari ambayo ilikua na kichwa cha habari “Male Groupie kicked out club for crying about unkown Artist “Diamond Platmumz” Hata hivyo ulishambuliwa na mashabiki wa Diamond na kwa asilimia kubwa na amini ni mashabiki wa nje ya nchi, kwa hali ya kawaida ni watanzania wachache ambao wanautaratibu wa kutembelea mtandao wa nje tena kama “Bossip”. Check hizo Comments
:

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.