Baada ya kuenea kwa uvumi wa muda mrefu kuhusiana na klabu ya Soka ya Simba kutaka kumrejesha kikosini golikipa wake wa zamani ambae alikuwa Yanga kabla ya kutibuana na viongozi wa klabu hiyo, Juma Kaseja team yetu ilibidi imtafute kufanya exclusive interview na Kaseja.
Juma Kaseja
ni golikipa aliyeichezea Simba kwa mafanikio kwa zaidi ya miaka
saba ila sasa yupo kama mchezaji huru licha ya taarifa za awali kusambaa
kuwa Kaseja kapelekwa Oman na baadhi ya viongozi wa Simba iliakajifue nakuja kuongeza nguvu kikosini, kabla ya taarifa nyingine kusema kuwa viongozi wa Simba wanavutana wapo wanaopenda arudi na wengine wanapinga.
“Watanzania
tumekuwa tukiongea sana kuliko vitendo mimi nafikiri Simba wana
magolikipa wao ambao wamewasajili sasa ingekuwa ni ajabu kumchukua
golikipa ambae hamjamsajili mnampeleka kwenda kufanya mazoezi ya
maandalizi halafu wale mliowasajili mnawaacha”>>>Kaseja
“Sijaenda
Oman, sikuwa Oman na wala sikuwa ndani ya nchi hii nilikuwa nje ya nchi
lakini nilichokifuata sipendi watu wajue ni maisha yangu
binafsi”>>>Kaseja
Zaidi msikilize Kaseja akikupa kiini cha tatizo la yeye kuachwa Simba

Note: Only a member of this blog may post a comment.