Kiungo wa kimataifa wa Rwanda anaekipa katika klabu ya Dar Es Salaam Young African (Yanga) Haruna Niyonzima August 7 amezungumza na team ya millardayo.com kitu gani kingine ambacho anaweza kufanya kwa ufasaha zaidi ya mchezo wa mpira wa miguu.
Niyonzima
ambae huwa ana uwezo mkubwa Uwanjani amesema anaweza kuimba muziki kwa
ufasaha na tayari kaimba nyimbo tatu kati ya hizo zinapigwa kwao, ila
anakiri kupenda kuimba na hawezi jua muziki unaweza utamfikisha wapi
licha ya kukiri kuwa anafanya kwa kujifurahisha tu.
“Kiukweli
napenda mpira ni kipaji lakini after football sometimes napenda kuimba
naamini pia nikiingia naweza kuimba sababu nishawahi kufanya majaribio,
nikisema nimejaribu kuimba ni kwamba nimeenda studio na sasa hivi na
nyimbo kama tatu”>>>Niyonzima
Ikumbukwe kuwa Haruna Niyonzima amejiunga na Yanga mwaka 2011 akitokea katika klabu ya APR ya Rwanda, Niyonzima ambae ni mahiri uwanjani amebahatika kupata watoto wakike mapacha Atika na Atifa April 17 2015.
Nimekusogezea sehemu ya Interview na wimbo aliomuimbia mama yake hapo chini!

Note: Only a member of this blog may post a comment.