Moshi Waziri Mkuu wa Zamani,
Edward Lowassa jana alidhibitiwa na polisi wakati alipokuwa akienda
kwenye msiba wa marehemu Peter Kisumo ambaye alizikwa jana katika Kijiji
cha Kighare mkoani Kilimanjaro.
Mara baada ya kufika kijijini hapo, magari ya polisi maarufu kama ‘Defender’ yalikutwa yakiwa yamekatisha Barabara ya Moshi- Same, na polisi wakiwa wamevalia kama vile walikuwa tayari kwa lolote, walisimamisha msafara huo. Kiongozi mmoja wa polisi katika eneo hilo aliwaambia wanasiasa hao kwamba hawakuruhusiwa kwenda msibani kwa staili ya msafara kwa vile hakukuwa na shughuli za kisiasa, hoja hiyo ilizusha malumbano yaliyodumu kwa dakika kadhaa. Lowassa na wenzake walipewa sharti na polisi kwamba waruhusiwe kwenda msibani huku waking’oa bendera zao lakini wafuasi wao warudi walikotoka, jambo ambalo Lowassa alilipinga na kuamua kugeuka na msafara wake kurudi Moshi.
Baada ya wananchi kukaidi, polisi
walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya, hali iliyozusha tafrani katika
mji huo mdogo ambao upo njia panda ya kwenda Taveta nchini Kenya.
Rais Jakaya Kikwete aliyekuwepo kwenye msiba huo, hakuzungumza chochote na badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiro, hata hivyo haikujulikana mara moja kwa nini rais hakuzungumza.
Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliposikia Lowassa kazuiliwa kufika, waliondoka kwenye kanisa lililopo Kivindo, katika Tarafa ya Usangi ambako ibada ya mazishi ilifanyika.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kilimanjaro, ACP Robert Boaz (pichani) alipoulizwa na gazeti hili kuhusu
kuzuiliwa kwa Lowassa na msafara wake alisema kwa wakati huo alikuwa
msibani.
“Kwa kuwa sasa nipo msibani siwezi
kuzungumzia tukio hilo,” alisema kamanda huyo na kukata simu. Mzee
Kisumo aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, alifariki dunia Jumanne iliyopita
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Note: Only a member of this blog may post a comment.