Saturday, August 15, 2015

Anonymous

HATARI SANA! Ikimpata straika huyu, SIMBA SC Bingwa!

SimbaWachezaji wa timu ya Simba wakishangilia.
Wilbert Molandi na Sweetbert Lukonge
KOCHA wa Simba, Dylan Kerr ametamba kikosi chake kimekamilika kila idara na endapo atapata nafasi ya kumsajili straika mwenye rekodi nzuri, hakuna kitakachoizuia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kerr raia wa Uingereza hakulificha Championi Jumamosi, kwani amesema, kila akikitazama kikosi chake anaona kimekamilika kuanzia mabeki, viungo na hata washambuliaji lakini akagutuka kitu kidogo tu.
“Timu yangu naiona imetimia kila idara, lakini kuna kitu kimoja kinaniumiza kichwa, nacho ni kusajili straika mmoja hatari mwenye uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho.
“Tena huyo mchezaji nataka awe na rekodi zilizo wazi kila mmoja ajue, siyo sifa za kuambiwa na watu! Huyo simtaki kabisa kwani hatokuwa na jipya,” alisema Kerr kwa msisitizo.


Ili kuonyesha kwamba hana utani, Kerr alisema: “Nina majina ya mastraika tisa kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kati yao ni mmoja tu nitakayemsajili baada ya kuridhika na sifa zake.”
Mastraika hao wanatokea nchi za DR Congo, Rwanda, Nigeria, Zambia, Botswana, Msumbiji, Ghana, Namibia na Afrika Kusini.
Huku akizungumza kwa umakini, Kerr alisema: “Bado naendelea kupitia rekodi ya kila mmoja wao na kujiridhisha na uwezo wao wa kufunga mabao kupitia Mitandao ya Wikipedia na Youtube, nikiridhika nitakuambia nani namsajili.”


Alisema mbali ya uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho, straika anayemuhitaji ni mwenye umri usiozidi miaka 28 kwani atakuwa bado na uwezo wa kupambana.
“Mawakala wanaendelea kunitumia majina na video za mastraika na kazi yangu ni kutazama yupi anafanya vizuri, halafu namchagua aliye bora kati yao,” alisema Kerr.


Kwa sasa, safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na Hamis Kiiza, Mussa Mgosi waliosajiliwa na hivi karibuni na Ibrahim Ajib. Katika mechi sita ilizocheza, Simba imefunga mabao 17 huku washambuliaji hao wakifunga mabao 10. Mgosi na Kiiza wamefunga matatu kila mmoja huku Ajib akifunga manne.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.