Mashaka Kisusi
NJEMBA wawili ambao ilisemekana ni wapiga debe, wamejikuta wakizichapa kavukavu wakigombea mzigo wa abiria.
Tukio hilo lililojaza watu ambao
walikuwa wakishangilia wakati njemba hao ambao majina yao hayakuweza
kupatikana mara moja wakizichapa, lilitokea hivi karibuni majira ya saa 6
mchana ndani ya kituo cha Mabasi cha Nyegezi, jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa hao
walitofautiana baada ya abiria mmoja kushushwa na daladala ambapo
walianza kugombea mzigo wake.
“Walikuwa wakigombea mzigo wa abiria
sasa huyu mwenye T-Shirt ya njano alionekana kumzidi nguvu mwenye
T-Shirt nyeusi, kuona hivyo, mwenye T-Shirt nyeusi alimtwisha mwenzake
kichwa cha uso hadi kumtoa nundu,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:
“Baada ya jamaa (mwenye T-Shirt nyeusi)
ku-’wini’ kihivyo, alimchukua abiria na mzigo wake wakaondoka na
kumuacha mwenzake (mwenye T-Shirt ya njano) akijichua nundu yake.
“Nundu ilikua kwa kasi kiasi cha
kuwafanya wapiga debe wenzake waanze kumcheka ambapo alipatwa hasira
sana akaanza kumsaka mwenzake ili alipize kisasi,” alisema shuhuda.
Hata hivyo, mashuhuda wakiwemo wapiga
debe wenzao, waliingilia kati kwa kumchukua mwenye T-Shirt nyeusi
kumpeleka eneo jingine na kumuacha mwenye T-Shirt ya njano akimtangazia
mwenzake kuwa hiyo vita haijaishia hapo, itaendelea siku nyingine!
Note: Only a member of this blog may post a comment.