Thursday, August 20, 2015

Anonymous

GOOD NEWS: Rais wa TFF atangaza majina ya wachezaji watano wa U-13 watakaojiunga na Orlando Pirates ya Afrika Kusini

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi August 20 ametangaza mpango wa kukuza soka la vijana na hii ni kama mrejesho wa mashindano yaliofanyika Mwanza kwa timu za watoto, Malinzi ameeleza mpango huo wa kuwaandaa vijana ambao watashiriki michuano ya mataifa ya Afrika U-17 yatakayofanyika mwaka 2019, Tanzania itakuwa timu mwenyeji hivyo imefuzu moja kwa moja.
DSC_0153
Hata hivyo Malinzi pia ametangaza kupatikana kwa wachezaji watano waliocheza michuano jijini Mwanza na August 29 wataelekea Afrika ya Kusini kufanya majaribio katika Academy ya klabu ya Orlando Pirates inayomilikiwa na Irvin Khoza. Majina ya wachezaji watano watakao ondoka kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Orlando Pirates ni Assad Ally Juma kutoka  Zanzibar, Maziku Amani, Issa Abdi kutoka Dodoma, Kelvin Deogratius kutoka Geita na Athumani Maulid kutoka Kigoma.

Sehemu ya wachezaji waliochaguliwa katika kikosi cha wachezaji 20
Sambamba na hayo Malinzi pia amethibitisha kuendelea na mipango ya kuomba nchi mbalimbali duniani ili kupata nafasi ya kuwapeleka wachezaji wa U-13 kujiunga na Academy za huko ili kukuza soka la vijana hao na kupata wachezaji watakaounda kikosi imara kwa michuano ya Afrika 2019 Tanzania.
Hii ni list ya wachezaji 20 waliochaguliwa katika kikosi cha U-13 kutoka katika michuano iliofanyika Mwanza
Malinzi 2 (1)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.