Mmiliki wa Lebo ya Aftermath Entertainment, Andre Romelle ‘Dr Dre’.
New York, Marekani
MMILIKI wa Lebo ya Aftermath Entertainment, Andre
Romelle ‘Dr Dre’, 50, ameibuka na kuwaomba radhi wanawake wote aliowahi
kuwafanyia mambo ya kikatili, akiwemo Michel’le ambaye alizaa naye mtoto
mmoja miaka ya 1990.
Dr Dre ambaye alitamba kinomanoma na Ngoma ya I Need a Doctor na
Still Dre, ameomba radhi kupitia mahojiano maalum aliyofanya na Jarida
la The New York Times wiki iliyopita.Dr Dre aliripotiwa kuwapiga wapenzi
wake wa zamani, Tairrie B aliyekuwa naye kwenye lebo moja na Michel’le
ambaye kipigo kilisababisha akawa na macho meusi na kumvunja mbavu.
“Ninawaomba radhi wanawake wote niliowafanyia mambo haya ya kikatili,
sikuwa na akili ya uelewa lakini sasa nimekua, najitambua kama mwanaume
bora.“Nikiwa na miaka 25 nilikuwa bado mdogo na nilikuwa nakunywa sana
pombe na kuwafanyia ukatili wanawake wangu, sikuwa na mpangilio wa
kimaisha.
“Nimeoa kwa miaka 19 iliyopita, ninajitahidi kuwa mwanaume bora
kwenye familia yangu. Ninafanya kila kitu ili nisionekane kama mtu yule
tena,” alisema Dr Dre ambaye amemuoa Nicole Young tangu mwaka 1996.

Note: Only a member of this blog may post a comment.