Friday, August 7, 2015

Anonymous

Dereva taxi mikononi mwa Sheria kisa Ubaguzi...Kagomea watu weusi wasipande gari..

1434941661931
Ubaguzini kitu ambacho kama ukikifanya alafu watu wakajua hivyo hakuna mtu atakuchukulia poa hata kidogo… imetokea mfululizo Marekani, Wamarekani weusi wameuawa na Maofisa Usalama na watu wakaingia Mtaani kulaani kwa nguvu, machafuko makubwa yakatiokea zaidi ya mara mbili!! 

Dereva wa Taxi New York Marekani kaangukia mikononi mwa Sheria, kamgomea mama mmoja Cynthia Jordan na watoto wake wawili wa kike kuingia kwenye Taxi akawajibu kwamba muda wake wa kazi umeisha, hatua chache mbele akakuta watu wengine ambao ni wazungu wawili akawapakia akaondoka nao. 

Mahakamani hawajachukulia poa hii kitu, dereva huyo wa taxi  Baqir Raza kaambiwa alipe faini ya Dola Elfu 10 kwa mwanamke huyo Cynthia Jordan na nyingine Dola Elfu 15 Mahakakamani kwa kosa hilo, hukumu ambayo hata mwanamke akiyebaguliwa karidhika nayo kabisa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.