Friday, August 7, 2015

Anonymous

Ahadi ya JK kwa wasanii, kinachomkera Khadija Kopa na wasanii kwenye semina ya TCRA..#255 (Audio)

Jana kulikua na matukio mawili makubwa katika tasnia ya Burudani, kwanza TCRA iliwaalika wasanii mbalimbali kwenye semina na pili wasanii walimualika JK ili kumuaga.
Kwenye 255 leo Afisa uhusiano wa TCRA Innocent Mungi amesema wasanii wamewaangusha kwa kushindwa kuhudhuria kwenye semina iliyoandaliwa kwa ajili yao ili kupewa mafunzi muhimu. na wao hawawezi kurudi nyuma na sasa wanakwenda kwenye makundi mengi na kama itawezekana kwa wasanii ni mpaka mwakani tena.

Meneja Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi
Kingine ni ahadi alizotoa Rais Kikwete wakati wa chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Mlimani City na ameahidi hata akiondoka madarakani bado ataendelea kuwa mlezi wa shughuli za wasanii kwani ni kazi ambayo haina gharama yoyote kwake..anatamani siku moja aone wasanii wanafika mbali kama kina Taylor Swift.

Khadija Kopa amesema kwenye tuzo za AFRIMMA hamhofii mtu yoyote kwa kuwa hakuna mtu atakayemuweza..anawaomba wasanii wenzake na wananchi wampigie kura ili aweze kushinda…kingine alichosema ni kuhusu kitu kinachomkera katika tasnia ya muziki kuwa ni vile vikundi vya pembeni vinavyopiga nyimbo zao mitaani na kuwakosesha wao ulaji.

Khadija Kopa
Wasikilize hapa kwenye 255 ya Clouds..

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.