Thursday, July 30, 2015

Anonymous

YANGA SC Imethibitisha Mkali Huyu wa Soka Anaondoka…Nani Atachukua Nafasi Yake? Shuka nayo hapa...

DSC_0256 
Ni siku kadhaa zimepita toka taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga Kpah Sherman zitoke kuwa anatakiwa na klabu moja  inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na kwa uhakika millardayo.com ilimtafuta katibu mkuu wa Yanga Dk. Jonas Benedict Tiboroha.

Tiboroha kathibitisha kuuzwa kwa Kpah Sherman kwenda katika klabu ya Mpulanga Black Aces kwa ada ya uhamisho ambayo haijwekwa bayana, ila mshahara amekiri atalipwa mara tatu ya aliokuwa analipwa Yanga, hata hivyo Tiboroha alithibitisha kutafutwa kwa mbadala wa Sherman na ukanda anaotokea.
Mpumalanga 
“Ni kweli Kpah Sherman hivi ninavyo ongea na wewe, nilikuwa naongea na agent wake kwamba amepata visa ya kuingia South Afrika kwa hiyo ataondoka leo kwenda huko kwa ajili ya kufanya test za afya ambayo kawaida huwa ni mchakato kabla ya mchezaji kusajiliwa kuingia timu yoyote kwa uhamisho wa kimataifa, ataondoka jioni anakwenda katika timu moja inaitwa Mpulanga Black Aces”>>> Tiboroha
Simba+waficha+jezi+picha 
” Ila kabla sijasema mbadala na sijui kama nitakwambia sasa hivi kwa sababu bado tupo katika hatua za mwanzo za maongezi hatujafikia Conclusion, kwa wenzetu wanaojua sheria sio kama sisi tunaingia mtaani hujaongea na klabu unaanza kusikia Yanga imemsajili fulani”>>>Tiboroha
mpumalanga 2 
“Nataka nikwambie tu, tuna mchezaji ambaye tupo katika maongezi naye atakuwa mbadala wa Kpah Sherman tutakapokuwa tumekubaliana na klabu yake pamoja na yeye mchezaji tutakuja public, anyway labda niwe wazi zaidi wako wawili mmoja anatoka Afrika Magharibi mmoja anatoka Afrika Mashariki”>>>Tiboroha

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.