Thursday, July 9, 2015

Anonymous

WATU Wawili Wafariki Katika Shimo la Choo Morogoro

Watu wawili wamekufa maji mjini Morogoro baada ya kuzama kwenye shimo la maji machafu wakati wakijaribu kuyatoa kwenye shimo la choo katika nyumba moja mtaa wa Kihonda B katika manispaa ya Morogoro.


Watu wawili wamekufa maji mjini Morogoro baada ya kuzama kwenye shimo la maji machafu wakati wakijaribu kuyatoa kwenye shimo la choo katika nyumba moja mtaa wa Kihonda B katika manispaa ya Morogoro. 

Eatv imeshuhudia askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wakivunja shimo la maji machafu kisha kutumbukiza ngazi na baadaye kutoa miili hiyo ya watu waliokufa maji kwa kutumia kamba.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema watu hao ni mafundi na walikuwa wakifanya kazi ya kuondoa maji machafu katika shimo la choo ambalo bado lilikuwa halijaanza kutumika.
Wamesema haikuweza kufahamika mara moja sababu ya watu hao kuzama huku wengine wakihisi pengine walikosa hewa. 

Nao baadhi ya wakazi wa mkoa wa Morogoro wakizungumzia tukio hilo wamesema ni vyema ifike mahali serikali iwajali watu kama hao ambao kuzibua vyoo kwa kuwa ndiyo ajira yao, wawezeshwe kupata vifaa maalum vya kuwasaidia kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walichukua miili na imepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa wa Morogoro
-EATV

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.