Thursday, July 9, 2015

Anonymous

Kikwete: Wasanii wa Bongo Fleva Wanatuliwaza Kwa Kuitangaza Tanzania Pale Tunapofanya Madudu Kwenye Soka

Rais Jakaya Kikwete amesema wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wameipeleka Tanzania mbali kwa kazi nzuri wanayoifanya na hivyo kuwaliwaza watanzania kwa kuwa nchi bado inaendelea kufanya ‘madudu’ kwenye soka la kimataifa.
Tanzania_Kikwete1_3259081b
Akihutubia bunge mjini Dodoma jioni hii, Kikwete amesema wasanii wanaliletea taifa heshima kubwa hivyo ni lazima wawezeshwe zaidi. 

Rais Kikwete amedai kuwa kwa kutambua umuhimu wa sanaa nchini, aliamua kuwaleta watu mashuhuri katika muziki nchini Marekani akiwemo mtangazaji wa E! News, Terrence J, meneja wa Ludacris, Shaka Zulu na producer David Banner ili kuja kuwapa elimu wasanii wa nyumbani.
Ameahidi kuwa atafanya mpango wa kuwaleta tena kwaajili hiyo na pia kutumia muda aliosalia madarakani kufanya awezalo kuwasaidia zaidi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.