Siku
zote nimeweka mdomoni neno linalosema kuwa mwanaume ni kifaa adimu kwa
sababu watu wanamaliza waganga, wanafanya matambiko ili wapate waume.
Cha ajabu kuna wanawake ambao Mwenyezi Mungu amewapa wanaume lakini
hawajitumi, wapo wapo tu!
Mfano, unakuta mume anafua mwenyewe, mume njaa inamuuma mke yupo anaangalia TV au kaenda kuzurura. Mume anavaa nguo chafu kisa mke hajali suala la kufua. Jamani mume kwa mke ni kama mtoto, anatakiwa ale kwa wakati, avae nguo safi.
Kuna baadhi ya wanawake wanadhani uzuri walionao na sifa zote walizojaaliwa kuwa nazo ni fimbo ya kumpigia mume.Kumbuka kuwa kuna wanawake wazuri sana kiasi kwamba ukiwaangalia wewe mwenyewe unawakubali lakini wanajituma ipasavyo kwa waume zao. Sasa wewe ni nani mpaka ubweteke hivyo?
Hebu jitahidi kumjali mumeo, isipite siku hujamjulia hali, kama yuko mbali na wewe mtumie hata ujumbe wa kumwambia kuwa umemkumbuka. Muulize amekula nini, mkumbushe kuwa muda wa kula umefika na sms nyingine za kuonesha kuwa umemkumbuka.
Utakuta mwanamke kutwa nzima anazurura, mara yuko Kariakoo anatafuta madera, mara kaenda kwa shosti wake Magomeni, akirudi nyumbani kachokaaa.Mume sasa anataka huduma unashangaa mke anadai kachoka, akifuatilia kachoshwa na kipi, eti sababu ya kuzurura kutwa nzima, huko ni kujiaibisha.
Mke kama ni mama wa nyumbani au umewahi kurudi kazini au uko ‘off’, tulia nyumbani ukimsubiri mumeo. Fanya usafi wa hapa na pale, kiandae chumba chako kwa kutandika kitanda, pulizia manukato, udi mzuri, asmini na kilua.
Mumeo akirudi akukute umeshajiandaa kimawazo kumpokea. Siyo anarudi anakuta nyumba iko vululuvululu, wewe mwenyewe unanuka jasho, utaachika kama siyo kutafutiwa mke mwenza shoga.
Lakini pia siyo mbaya ukatenga muda wa kumkata kucha mumeo, kumsafisha masikio kwani mbali na kwamba kufanya hivyo ni kumfanya awe msafi, pia kunaamsha hisia.Mwisho nakukumbusha mwanamke mwenzangu kwamba fanya yote lakini tendo la ndoa ni haki ya mumeo na ni mhimili wa ndoa.
Kilichokufanya ukaaicha familia yako na kwenda kwa mume siyo kula wala kufuata mali, umefuata haki hii. Kwa maana hiyo basi, isitokee hata siku moja ukamwambia mumeo; ‘nimechoka’ wakati yeye anahitaji.
Hii kusema mara unaumwa, mara umechoka, mara hujisikii ni kosa kubwa na wengi wamejikuta wakitafutiwa michepuko kwa kutokuwa makini katika kuwatimizia waume zao.
Kumbuka kwamba, licha ya uzuri wako na kujaaliwa kuwa na umbo zuri, usilete maringo kwa mumeo. Uzuri wako hauwezi kuishika ndoa, wajibika kama mke ili umfanye mumeo aamini amepata mke kwa maana halisi ya mke na siyo toi, upo hapo shoga?

Note: Only a member of this blog may post a comment.