Imelda Mtema, Zanzibar
Staa mwenye jina kubwa
duniani kutoka Sauzi, Leleti Khumalo ‘Sarafina’ amewafunda mastaa wa
kike kwa kuwataka wajitume ili kujiletea maendeleo kwa kuwa muda wa
kutumiwa kingono na wanaume umepita.
Akizungumza na Ijumaa mjini hapa akiwa mmoja wa wasanii waliohudhuria Tamasha la Ziff, Sarafina aliseme kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakijiweka nyuma na wakati mwingine kukubali kutumiwa kingono ili watoke wakati uwezo wanao.
“Hapa Afrika waongozaji wa filamu wa kike ni kama hamna wapo wachache sana, wanawake wanahitaji kusimama na kufanya kazi zao wenyewe, muda wa kutumiwa kingono umepita, amkeni mfanye kazi wanawake wenzangu,” alisema Sarafina.

Note: Only a member of this blog may post a comment.