Brighton Masalu
MUIGIZAJI aliyekuza jina kupitia Filamu
ya Misukosuko, Salama Salimin ‘Sandra’ amesema sababu iliyomfanya kukaa
kimya kwenye uigizaji ni malipo na kipato kidogo hivyo kuamua kutafuta
riziki kwa njia nyingine (hakuzitaja).
Akizungumzia maisha yake kwa sasa,
msanii huyo asiye na makuu alisema hamaanishi kazi ya sanaa haina
masilahi, isipokuwa kwa upande wake aliona hapati kile alichokihitaji
licha ya kuwa na kipaji halisi cha uigizaji.
“Unajua ni lazima uwe na mikakati mingi
katika kutafuta maisha, huwezi kung’ang’ana na kitu kimoja tu, kwa
upande wangu filamu hazinilipi kama ninavyohitaji, ndiyo maana nikaamua
kukaa pembeni kwanza, lakini simaanishi kuwa kazi ya sanaa haina
masilahi, la hasha ila ni maoni ya upande wangu,” alisema Sandra.

Note: Only a member of this blog may post a comment.