Thursday, July 23, 2015

Anonymous

Ndoa ya Amini imempoteza kwenye game? Collabo ya Sauti Sol na WaTZ, ajali ya Jambo Squad..255 (Audio)

Kuna uhusiano wowote wa ndoa na staa kushuka kimuziki? Amini amefunguka kwenye 255 na kusema kwa upande wake haamini kuwa ukioa kipaji chako kinashuka..yeye binafsi anasema anashukuru kumpata mke ambaye wanaendana katika kazi zake

Amesisitiza pia kutosikika kwake mara kwa mara ni lazima wasanii kupeana nafasi kama kundi la THT si kila muda kunatoa nyimbo.

Amini na mke wake siku ya Harusi
Sauti Sol wanatamani kuungana na kufanya muziki pamoja..wamesema kufanya collabo kwa kushirikiana watafika mbali..wamesema tayari wameshirikiana na Wuesi, Ommy Dimpoz,Vanessa na hivi karibuni watatoa collabo na Ally Kiba.

Sauti Sol
Jambo Squad walipata ajali wakati wakienda kwenye shoo Babati..wakiwa njiani maeneo ya Tarangire wakati dereva akiwa kwenye mwendo kasi walikutana na lori, dereva akaamua kulikwepa na kukosa control na kujikuta wakiwa wamepata ajali mbaya.

Kwa sasa bado hawapo vizuri kutokana na kuumia sehemu mbalimbali za mwili huku baadhi yao waliokuwa kwenye gari moja wakiwa hawana fahamu mpaka sasa.

Kundi la Jambo Squad
Wote wamesikika hapa…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.