Dirisha la usajili wa kipindi cha kiangazi limefunguliwa leo rasmi na klabu ya Liverpool imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine baada ya Firmino kuungana na Kikosi hicho wiki iliyopita.
Liverpool wamemsaini Nathaniel Clyne kutoka Southampton kwa ada ya uhamisho ya Pound Milioni 12.5, mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka 5.
“Nina furaha kutimiza ndoto yangu ya kuja hapa Anfield kuitumikia klabu kubwa kama hii,” Clyne amenukuliwa na mtandao wa Liverpool.
“Baada ya Liverpool kuonesha kunihitaji, nilifurahia na nikapenda uhamisho huo ukamilike haraka.“>>> Clyne.

Note: Only a member of this blog may post a comment.