Kuna mastaa wengi duniani tunaowajua na
kuwapenda sana, na kuna wengine tunatamani kuja kuwa kama wao. Lakini
sio kila kitu kuhusu mastaa hawa tunavijua, wengi tunawapenda lakini
kuna vitu flani kuhusu wao hatuvijui.
Nimekusogezea picha kumi za mastaa kutoka Marekani, kila mmoja ana kitu chake ambacho labda umewahi au hujawahi kukisikia.

Television superstaa na millionea Oprah Winfrey wengi
tunamfahamu kupitia kipindi chake Oprah Winfrey Show. Lakini maisha
yake hayakuwa ya furaha na amani akiwa mtoto, akiwa na miaka 9 aliteswa
na ndugu zake na alipokuwa na miaka 14 alibakwa na kupewa mimba na
binamu yake, mtoto wake alikufa alipojifungua.
Rappa maarufu duniani Jay Z ni
miongoni mwa mamilionea wakubwa kwenye Industry ya muziki wa Hip Hop.
Lakini na yeye hakuwa na maisha mazuri kwani utotoni aliishi maisha duni
sana jijini Brooklyn na alishawahi kumpiga kaka yake risasi akiwa anajaribu kumuibia hela.
Rappa Lil Wayne ni miongoni mwa marappa wakubwa pia duniani, akiwa chini ya lebo ya Cash Money Records
Lil Wayne anafahamika kwa ngoma nyingi kali lakini rappa huyu ana
watoto wanne na wanawake wanne tofauti, amabao hajafunga nao ndoa.
Busta Rhymes ni msanii mwingine maarufu wa Hip Hop anaejulikana kwa kwa style yake tofauti ya kuimba. Busta Rhymes na rappa Jay Z walisoma shule moja na kupanda basi moja la shule.
Nicki Minaj ni rappa mkubwa alianza kutengeneza headlines kubwa miaka ya 2008-2009 kwenye entertainmnet industry na yupo chini na ya Cash Money Records. Lakini Nicki Minaj ana ugonjwa unaoitwa Acrophobic, ugonjwa wa uwoga wa kupanda majengo marefu.
RnB pop queen Jenifer Lopez
ni miongoni mwa wasanii wakubwa katika industry ya muziki duniani,
akiwa na zaidi ya rekodi millioni 50. Na katika historia ya wanamziki
JLo ana historia ya kuwa na movie na wimbo zilizoshika namba moja kwenye
wiki moja.
Leona Lewis, Jessie J na Adele
ni wasanii kutoka Uingereza walioweza kupenya na kutikisa soko la
muziki Marekani na kupata mamilioni ya pesa kupitia nyimbo zao. Kizuri
zaidi ni kwamba wasanii hawa watatu walisoma shule moja,The BRIT School of Performing Arts and Technology mwaka 2006 Croydon nchini Uingereza.
Gwen Stefani ameshinda idadi ya tuzo za Grammy sawa na wasanii Nas, 50 Cent, Busta Ryhmes na Drake.
Kabla ya kuanza kuimba rasmi, msanii maarufu wa Hip Hop P Diddy alikuwa back-up dancer wa Big Daddy Kane na Heavy D.
Baada ya kufanya maamuzi ya kufanya muziki msanii wa Pop Marekani Madonna alihamia jijini New York kutimiza
ndoto zake, lakini mambo hayakwenda kama anavyotarajia, alijikuta
anafanya kazi ya uhudumu kwenye restaurant mbali mbali jijini hapo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.