Hamida Hassan
MWANAHARAKATI na mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria kwa kutambua adha wanazokutana nazo akina mama kwenye ndoa zao, ameandaa pati maalum kwa ajili ya kuwafunda, Risasi Jumatano linakupasha. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Joyce alisema pati hiyo ameipa jina la Djuju na ni mategemeo yake kuwa itaungwa mkono na wanandoa wote kwani lengo lake ni kutoa elimu na kuwakumbusha wajibu wao.
“Nataka niwaelezee wanandoa hasa wanaume kuwa mwanamke ana kitu anachokifuata kwa mume, siyo vipigo kama wanavyokutana navyo wanawake wengine, mfano yule aliyemwagiwa uji, aliyekatwa mguu na mume wake na wengine wengi. Wanafuata upendo na siyo ukatili katika ndoa,” alisema Joyce.
Alisema mipango yote ya shughuli hiyo imeshakamilika na kwamba muda siyo mrefu atatangaza sehemu ambayo pati hiyo itafanyika na kuwataka wote wenye matatizo katika ndoa zao kujiandaa kwenda kukumbushwa jambo hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.