Usiku wa jana kuamkia leo July 19 2015 Diamond Platnumz kanyanyua ushindi mwingine kwenye Tuzo za #MTVMAMA2015, zilizokuwa zikitolewa Durban Africa Kusini.
Leo Diamond alipost Video inayomwonesha staa wa Mitindo Bongo, mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akicheza wimbo wa ‘Mdogomdogo‘ alafu akaandikia hivi >>>> ‘Mbona Bado, Mtanyooka tu..‘ >>>> @ diamondplatnumz
Baadae Jokate nae akaandika kwenye ukurasa wake wa @Instagram kuhusu video hiyo ambayo alimpost Diamond.
==>>Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni #TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukuma akani-record na kumtumia @diamondplatnumz
bila mimi kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua
baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio
dhambi kucheza mziki wowote uupendao. Ila kitendo cha @diamondplatnumz
kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo
najiuliza maswali mengi 1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia
ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi
wake ni sifa kwa taifa ila 2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado
Mtanyooka? Ili amkomoe nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficial
anatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na
kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na
kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life 3, Pengine
ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa
nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu
dangote. Which to me is just dead wrong. @diamondplatnumz
hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa
Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya
tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi
kutugeuka. Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef
unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha
wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka
kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea
kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo
kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga
maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila
ungetumia busara kidogo. Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie
fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila @babutale
hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo?
Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu
atatunyanyua. 🙏

Note: Only a member of this blog may post a comment.