Pata picha mtu anajiamini kabisa
anaanzisha Kituo cha Polisi, anafanya kila kitu kama Polisi
wanavyofanya.. kuna pingu, sare za Askari, Silaha… unaambiwa mpaka gari
yake ina king’ora juu kama gari ya Polisi kabisa, lakini kila kitu ni
feki na jamaa amepiga kazi kwa miaka miwili hakuna aliyemshtukia Kituo
hicho feki cha Polisi.
Ishu ilikuja kushtukiwa baada ya mpenzi
wake na jamaa huyo kuamua kuripoti Polisi kwenyewe, jamaa wakamfatilia
mpaka wakamkamata.
Mchina huyo anajiita Lei,
alikorofishana na mpenzi wake, katika majibizano yao ikaonekana jamaa
anatishia kuisambaza mitandaoni video inayoonesha wakiwa wanafanya
mapenzi.. mwanamke akaona isiwe tatizo, akaenda moja kwa moja Polisi
kuripoti.
Lei
alikuwa akifanya mishemishe zake hizo Jimbo la Hubei China kwa muda
wote mpaka alipokamatwa, jinsi ambavyo alijikamilisha wapo ambao aliwahi
kuwakamata kabisa na kuwatoza faini ili mambo yaishe juujuu, mwishowe
amekutana na Polisi wenyewe… stori za kukamatwa kwake zimechukua sana
headlines mitandaoni, wengi wamejiuliuza imekuwaje akafanya kazi yake
feki miaka miwili bila kukamatwa?

Note: Only a member of this blog may post a comment.